Ombi hilo wamelitoa kwa mkuu wa mkoa wa tanga Martin Shigela katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
Wamesema ulipaji wa fidia ukifanyika mapema utawasaidia wananchi kuanza maandalizi ya kuanzisha miradi ambayo itaendana na mahitaji ujio wa mradi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.
Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa mkoa amewapongeza wananchi kwa uvumilivu wao na kuwatoa hofu kuhusu ulipwaji wa fidia na kwamba wakati ukifika kila mmiliki wa eneo atalipwa haki yake kulingana tathimini iliyofanywa.
No comments:
Post a Comment