Monday, July 17, 2017

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa
Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewataka Wakenya kuvumiliana wakati huu ambapo taifa hilo linakaribia uchaguzi.
Akizungumza nchini Kenya katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa usalama nchini humo marehemu Joseph Nkaiserry, Lowassa amesema kuwa kenya inapaswa kujifunza kutoka kwa machafuko ya uchaguzi ya mwaka 2007.
Matamshi yake yaliungwa mkono na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliyewataka wafuasi wake na wale wa kiongizi wa upinzani Raila Odinga kuvumiliana.Rais wa Kenya Uhuru KenyattaUhuru alisema kuwa hakuna haja ya kupakana tope za matusi akiongezea kuwa matusi hayasaidii.
''Sisi sote ni Wakenya , hatuna taifa jingine la kujenga baada ya uchaguzi ,tunaomba amani, amani amani'', alisema rais Uhuru Kenyatta.
Matamshi ya Uhuru na Lowassa yanajiri wakati ambapo wafuasi wa upinzani na wale wanaounga mkono serikali wamekuwa wakiwazomea viongozi wanaotoka pande pinzani katika mikutano ya kampeni na hata kusababisha mikutano hiyo kusitishwa.
Lowassa amesema kuwa Kenya ni tegemio la kiuchumi katika mataifa ya Afrika mashariki hivyobasi inafaa kuwa mfano kwa kuhakikisha kuwa taifa hili halijiingizi tena katika jinamizi la machafuko yalioonekana miaka 10 iliopita.
''Ombeni musirudi katika mapigano yaliotokea mwaka 2007, Kenya iko mbele kushinda taifa lolote lile Afrika mashariki na tunataka muendelee kusonga mbele.Marehemu Jenerali Joseph Nkaessary alikuwa waziri wa usalama nchini KenyaLowasa alisema kuwa marehemu Nkaissery aliamini sana Umoja wa Afrika mashariki na alijitolea kufanya kazi na akawataka viongozi wengine kuiga mfano wake.
Naye rais Uhuru aliongezea kwamba Kenya na Tanzania ni pacha na zitaendelea kuimarisha ushirikiano wao kwa lengo la kurahisisha biashara na usalama kati ya raia wa mataifa hayo mawili.
Miongoni mwa wale waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga na naibu wa rais William Ruto

Msafara wa rais Mugabe wahusika katika ajali ya barabarani

Rais Mugabe akiwa katika gari lake
Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe alipata majeraha madogo katika ajali ya barabarani, lakini rais Mugabe hakuumia popote.
Vyombo vya habari vya serikali vinasema ajali hiyo ilitokea wakati familia hiyo ilipokuwa ikitoka uwanja wa ndege wa Harare.
Walikuwa wamerudi kutoka Singapore ,ambapo rais huyo ameenda kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.
Kulingana na mwandishi wa BBC nchini humo Shingai Nyoka mke wa rais Grace Mugabe alipata jeraha katika mkono wake katika kile serikali inasema ni ajali ndogo ya barabarani iliohusisha msafara wa rais.
Bi Mugabe alitibiwa katika kliniki moja na kuruhusiwa kwenda nyumbani bila majeraha makubwa.
Msemaji wa rais aliambia chombo cha habari cha serikali kwamba mke wa rais alilalamikia uchungu katika mkono wake lakini hakuelezea kiini cha ajali hiyo.
Shahidi mmoja anasema kuwa aliona mwili uliotengwa wa mwendeshaji pikipiki wa msafara wa rais katika eneo hilo.
Kumekuwa na makumi ya ajali yanayohusisha msafara huo wa rais katika kipindi cha miaka mitano iliopita.
Msafara huo una magari 10 yenye ving'ora vya kuyaonya magari mengine.

Sunday, July 16, 2017

Acacia yakubali kuilipa Tanzania

rais
Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imekubali kuilipa serikali ya Tanzania nyongeza ya mrabaa wa kati ya asilimia 4 mpaka 6 kama ilivyoainishwa kwenye muswada wa sheria mpya ya madini nchini humo.
Serikali ya Tanzania na kampuni ya Acacia ziliingia katika mgogoro mapema mwezi tatu mwaka huu kutokana na kuzuiliwa kwa makontena 256 ya Mchanga wa dhahabu (makinikia) kwenye bandari ya dar es salaam baada ya kubainika kuwa Acacia haitoi taarifa sahihi ya kiwango cha madini kilichopo katika mchanga huo hivyo kulipa tozo zisizo sahihi kwa karibu miongo miwili jambo ambalo linapingwa vikali na kampuni hiyo.
Licha ya kukubali kulipa ongezeko hilo Acacia imesema bado inaendelea kutathimini athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na kuundwa kwa sheria hiyo mpya.

Saturday, July 15, 2017

Watu 8 wamefariki katika mkasa cha kukanyagana nchini Senegal

Ukuta ulioporomoka ulikuwa umeunganishwa na viti vya kukalia uwanjani
Duru kutoka Senegal, zinasema kuwa watu wanane wameuwawa katika kisa cha kukanyagana, baada ya vurumai kutokea wakati wa mchuano wa mechi ya kandanda, kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar.
Shirika rasmi la habari la serikali ya nchi hiyo- (APS), linasema kwamba mashabiki wa timu mbili za soka, walikabiliana baada ya mchuano wa soka uliochezewa katika uwanja wa michezo wa Demba Diop stadium, kumalizika.
Ukuta uliporomoka wakati ambapo idadi kubwa ya watu walipokuwa wakiondoka kwa kasi uwanjani.
Nyavu ya goli iliyoharibiwa baada ya kutokea kwa rabshaIdadi kubwa mno ya watu wamejeruhiwa.
Kisa hicho kilitokea wakati wa fainali ya kuwania kombe la ligi kuu nchini humo, kati ya timu ya soka ya Stade de Mbour na Union Sportive Ouakam.
Mapigano yalianza kati ya mashabiki wa timu hizo mbili hasimu, hatua iliyowachochea maafisa wa polisi kuwarushia vitoa machozi. Hatua hiyo ilisababisha taharuki kubwa miongoni mwa mashabiki ambao walianza kukimbia na kusababisha mkanyangano, na kuporomoka kwa ukuta.
Baadhi ya mashabiki walirusha kila aina ya vifaa yakiwemo mawe.Ramani ya taifa la SenegalPicha zinazosambazwa mitandaoni, zinaonesha watu wakikurupuka na kujaribu kupanda juu ya ukuta mfupi, huku wakizungukwa na wingu kubwa wa moshi wa vitoa machozi.
Runinga ya taifa ya nchi hiyo, inasema kuwa, magari ya huduma za dharura na vikosi vya zima moto vilifika maeneo ya tukio hilo.

Wednesday, July 12, 2017

Nusura ndege ya Canada igonge ndege nne uwanjani San Francisco

Air Canada planes. Archive photo
Idara inayohusika na safari za ndege nchini Marekania FAA ,inachungunza kisa ambapo ndege ya shirika la Air Canada nusura igonge ndege zingine katika uwanja wa San Franciso.
Shirika hilo linasema kuwa ndege ya AC759 ikitokea Toronto iliruhusiwa kutua siku ya Ijumaa lakini rubani akajianda kutua katika barabara ambapo ndege zingine zilikuwa zinajianda kupaa.
Waelekezi wa safari za ndege waliweza kufahamu tatizo hilo na kumuamrisha rubani kupaa tena ili kujiandaa kutua kwa kwa mara ya pili.Kisha ndege hiyo ikaweza kutua salama.
FAA kwa sasa inachunguza umbali uliokuw kati ya ndege ya Air Canada na ndege iliyokuwa ikijiandaa kupaa.
Kisa hicho kinatajwa kuwa kisicho cha kawadia.
Air Canada inasema kuwa abiria 135 na wahudumu 5 walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Haijulikani ni watu wangapi waliokuwa ndani ya ndege nne zilizokuwa kwenye barabara ya kupaa.

map
Nusura ndege ya Canada igonge ndege nne uwanjani San Francisco

Makamu Rais Yemi Osinbajo amtembelea Buhari London

Muhammadu Buhari na makamu Rais Yemi Osinbajo Abuja Machi 13,2017Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambae yuko London kwa ajili ya matibabu, amefanya mkutano wake wa kwanza na anaye kaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili sasa.

Msemaji wa kaimu Rais, Yemi Osinbajo, ameelezea kuwa mkutano huo ulikuwa mzuri.
Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi.
Buhari alirejea kazini mwezi Machi baada ya matibabu London
Buhari amekuwa jijini London tangu mwezi Mei, akipata matibabu kwa ugonjwa ambao haujatajwa.
Bwana Osinbajo anategemewa kurudi nchini Nigeria baada ya mkutano huo.
 Ukimya wake umeibua mjadala nchini Nigeria iwapo Buhari ataweza kurudi na kuendelea na majukumu yake ama la.
Buhari akiwa na familia yake mwezi Machi
Buhari akiwa na familia yake mwezi Machi

Trump ashtakiwa kwa kuwazuia wakosoaji katika Twitter

A picture showing the masthead of President Donald Trump's @realDonaldTrump Twitter account
Rais wa Marekani Donald Trump kwa muda wa miaka 30 amekabiliwa na zaidi ya na kesi 4,000
Na sasa mwanabiashara huyo ambaye sasa ni Rais, ameshtakiwa kwa mara nyingine, baada ya watu saba kumshtaki kwa kuwazuia kwenye akaunti yake ya twitter.
Bwana Trump ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijami ambayo anaituma kuwapongeza washirika na kuwashambulia mahasimu wake.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na taasi ya Knight First Amendment Institute, ambalo ni kundi la kupigania uhuru wa kusema katika chuo cha Columbia.
Watumiaji hao saba walisema kuwa akaunti zao zilifungwa na rais au wasaidizi wake, baada ya wao kukejeli au kukosoa ujumbe alioandika Trump.
Watumiaji wa Twitter hawan uwezo wa kuona au kujibu ujumbe katika akaunti zinazowazuia.
Mashtaka hayo ni kuwa kwa kuwazuia watu hawa, Bwana Trump amewazuia kujiunga na majadiliano ya mtandaoni.

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...