Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambae yuko London kwa ajili ya
matibabu, amefanya mkutano wake wa kwanza na anaye kaimu nafasi hiyo kwa
miezi miwili sasa.Msemaji wa kaimu Rais, Yemi Osinbajo, ameelezea kuwa mkutano huo ulikuwa mzuri.
Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi.

Buhari amekuwa jijini London tangu mwezi Mei, akipata matibabu kwa ugonjwa ambao haujatajwa.
Bwana Osinbajo anategemewa kurudi nchini Nigeria baada ya mkutano huo.
Ukimya wake umeibua mjadala nchini Nigeria iwapo Buhari ataweza kurudi na kuendelea na majukumu yake ama la.
![]() |
| Buhari akiwa na familia yake mwezi Machi |

No comments:
Post a Comment