Thursday, July 6, 2017

Mamba mto Ruvuma tishio, Serikali yaombwa kuchukua hatua

Mamba--620x309Wakazi wa vijiji kumi vya halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambavyo vipo kando kando ya Mto Ruvuma wameiomba serikali kuwaondoa mamba wakubwa walio katika mto huo ambao wanaua watu na kujeruhi na kwa mujibu wa takwimu zilizopo kuanzia mwaka 2010 hadi sasa, mamba hao wameua watu kumi na tisa na kujeruhi kumi na watano.
Mwandishi wetu Adam Malima aliyeko mkoani Mtwara amefuatilia taarifa hiyo na hapa anaripoti zaidiÖ..
Hakuna namna yoyote ya kuacha kufika katika mto Ruvuma ambao una mamba wanaokamata watu, kukosekana kwa maji ya bomba vijijini mwao vinawafanya wakazi wa vijiji jirani kutumia maji ya mto huo kwa matumizi yote ya binadamu.
Tayari watu kumi na tisa wameripotiwa kuuawa na mbamba katika mto huo huku wengine wakipata majeraha na ulemavu wa kudumu.
Hamisi Mpunga ni mtoto na mkazi wa kijiji cha Sindano aliyejeruhiwa na mamba kwenye mkono wake wa kuume tangu mwaka 2013 akiwa anavua samaki anaugulia maumivu hadi sasa,huku wazazi wake wakikosa uwezo wa kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.
Serikali inaombwa kuwasaidia wakazi hao ili wasiendelee kuzulika na mamba katika mto wanaoutegemea kwa maji ya kunywa na shughuli za kilimo.
Licha ya uwepo wa mamba katika mto huo watoto wanaogelea bila uwoga

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...