Thursday, July 6, 2017

Mabweni yateketezwa Hanang, Yatumika na wanafunzi wa Madrassa

Image result for mabweni ya teketea motoKamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara chini ya Mkuu wa wilaya hiyo ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo imetekeza mabanda zaidi ya 12 yaliyokuwa yakitumika kama mabweni ya wanafunzi waliokuwa wakipata mafunzo ya dini ya kiisilamu katika chuo cha Madrasa Albadri ambacho kimeanzishwa kinyamela katika pori lililopo kata ya Diloda tangu mwaka 2008 huku pia ikibainika mmiliki wa chuo hicho kukiuka haki za binadamu kwa kuwatumikisha watoto walio chini ya umri kwa kuwalimisha mashamba, na wengine wawili kupoteza maisha katika kipindi cha mwezi may mwaka huu baada ya kutumbukia katika rambo lilochimbwa katika eneo hilo kwa ajili ya kuhifadhi maji pindi mvua zinaponyesha .
Eneo hili ndilo la chuo na huu ni muonekano wa mabweni ya chuo hiki kabla ya zoezi hili la utekezaji lakini shimo hili ambalo linaelezwa kuchimbwa na chuo hiki kwa lengo la kutwamisha maji pindi mvua inaponyesha kwaajili ya matumizi ya kila siku ikiwemo kunywa ambapo kwa sasa linaoneka kukauka ndipo yalipoishia maisha ya Yusuph Ibrahimu aliyekuwa mwanafunzi wa hapa kutoka wilaya ya kondoa lakini pia maisha ya Saidi Mashaka kutoka eneo la Galapo wilaya ya babati yaliweza kuishia hapa na huyu ndiye mmiliki wa chuo hik ambaye nib wa Saad Suleiman mkaazi wa babati mjini.
Viongozi wa dini nao wakatoa maneno yao ikiwemo baraza la waisilamu Tanzania Bakwata wilaya ya Hanang juu ya kitendo cha uanzishwaji wa chuo hiki na utumikishwaji wa watoto.
Sara Msafiri Aly yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya ya hanang lakini ni mkuu wa wilaya hii.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...