Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti yakiwemo ya kukutwa na dawa za kulevya na pembe za ndovu zenye thamani zaidi ya shilingi million 33.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema askari wakiwa katika doria walipokea taarifa kutoka kwa raia wema walifanikiwa kumkamata Kibosa Kibona mkazi wa Mlali wilayani Mvomero ambapo amekutwa na pembe za ndovu mbili zenye thamani zaidi ya shilling million 33.
katika tukio lingine kamanda matei amesema jeshi la polisi limefanikiwa kumukamata Sande Balinusi maeneo ya Msamvu manispaa ya morogoro baada ya kumpekua na kukutwa na kiloma moja ya dawa za kulevya aidha watuhumiwa wao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment