Wito huo umetolewa na mkuu wa gereza la mahabusu Sumbawanga mara baada ya kupokea msaada wa mahitaji ya kibinadamu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa akiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo akikabidhi msaada huo, amewapongeza askari wa jeshi la magereza kwa kazi ngumu wanayoifanywa kuhakikisha wafungwa wako salama wakati wote na kueleza nia ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kalambo kufika gerezani hapo.
Vitu vilivyokabidhiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kalambo kwa mkuu wa gereza la mahabusu Sumbawanga, baadhi yake ni sabuni, miswaki, dawa ya meno, mafuta ya kupakaa, nyembe na kalamu za kuandikia maaskari wawapo kazini.
No comments:
Post a Comment