Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limewafikisha mahakamani watu wanane wote wakazi wa mkoa huo na mmoja kutoka Pemba kwa tuhuma ya kukusanya watoto na kuwa fungia ndani ya nyumba kwa muda mwezi mmoja kwa lengo la kuwasafirisha.
Sintofahamu ya kuwapo kwa taarifa za kundi la watoto ambao wamekuwa wakifungiwa ndani kwa siku kadhaa katika moja ya nyumba katika eneo la Kichangani kata ya Chanji wilayani Sumbawanga, ambapo raia wema walitoa taarifa polisi, jeshi la polisi limedai kuwa limewafikisha mahakamani watuhumiwa nane baada ya kukamilisha upelelezi.
Baadhi ya wananchi wamelaani kitendo cha watuhumiwa kuwasafirisha watoto hao bila kufuata utaratibu kwa lengo ambalo bado halijawekwa wazi na watuhumiwa
Watuhumiwa nane wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kusafirisha binadamu kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment