Friday, July 7, 2017

Mchanga wa madini ya dhahabu Hanang, DC apiga marufuku kusafirisha kwenda Mwanza

imagesMkuu wa wilaya ya Hanang Sara Msafiri amepiga marufuku usafirishaji wa udongo pamoja na mchanga unaosadikiwa kuwa na madini ya dhahabu na kuepelekwa nje ya wilaya hiyo ambapo unapelekwa jijini mwanza kwaajili ya utafiti bila kushirikisha serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya na kuagiza kampuni ya Kudu ya Jijini Arusha kuwasilisha ripoti ya tadhimini juu ya utafiti wa madini ya dhahabu inayofanywa na kampuni katika eneo la Basotu wilayani hapo.
Ni marufuku inayotekeleza agizo la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kutaka shughuli zote za uchimbaji wa madini pamoja na utafiti wake kuwa chini ya kamati za ulinzi na usalama ya maeneo husika ambapo mkuu wa wilaya ya hanang anatoa maagizo haya kwa kampuni ya Kudu Resource Kampani ya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Basotulengo likiwa ni kuepusha migogoro mbalimbali baina ya wananchi na wawekezaji katika maeneo ya machimbo.
Nao uongozi wa basotu wakatoa ushauri huu kwa serikali wakilenga zaidi kwa rais.

Hivi karibuni inaelezwa wananchi wamevamia eneo hili kwa kuitaka kampuni hii kutekeleza baadhi ya ahadi zake kwa wananchi wa eneo la basotu ambazo waliziahidi kabla ya kuanza kwa utafiti ambapo ni pamoja na barabara,na kuchimba visima vya maji kwaajili ya wakaazi wa basotu.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...