Saturday, July 8, 2017

Marufuku ya ushuru wa mazao, Iringa waeleza wasiwasi wa msamaha huo

unnamed (9)Kutokana na serikali kutangaza kufuta ushuru wa mazao kwa magari yanayobeba mizigo chini ya uzito wa tani moja halmashauri za wilaya mkoani Iringa zimeingia wasiwasi kuwa msamaha huo unaweza kutumiwa vibaya na wafanyabiashara wakubwa kupitisha mizigo yao kidogo kidogo kwenye vizuizi vitumikavyo kukusanya ushuru kwa lengo la kukwepa tozo hizo.
Baadhi ya wajumbe wa jumuiya ya serikali za mitaa nchini ALAT mkoa wa iringa wameelezea wasiwasi wao katika kikao cha Jumuiya hiyo kilichofanyika wilayani kilolo ambako baadhi ya madiwani akiwemo Mstahiki Meya wa manispaa ya iringa Bw Alex Kimbe wanabainisha ya kinachoweza kutokea endapo jambo hilo litabaki kuwa hivyo.
mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Iringa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Bw Charles Makoga anasema pamoja na kupoteza mapato kwenye eneo hilo la ushuru wa mazao pia halmashauri zitegemee mtikisiko wa kukosa makusanyo kutokana na ushuru wa mabango kuhamishiwa TRA huku kodi za majengo nazo zikiendelea kukusanywa na mamlaka hiyo ya mapato.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...