Watu wa jamii ya kifugaji katika kata ya Ngolie wilaya ya Ngorongoro wamefanya maandamano kwenda ofisi ya kata hiyo kulalamikia ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni thelathini za ujenzi wa zahanati zilizotolewa na serikali kupitia baraza la wafugaji zinazo daiwa kuliwa na baadhi ya viongozi wa kaya hiyo. Wakazi hao wamesema wamefika hatua hiyo kwakuwa kata yao haina zahanati licha ya serikali kumetoa fedha ili kusogeza karibu huduma ya afya kwa wananchi lakini wajanja wachache wametumia vibaya fedha hizo ambapo sasa wanaiomba serikali kuungilia kati.
Viongozi wa mila kutoka jamii ya kifugaji wamesema wapo tayari kutoa ushirikiano kwa serikali kwa lengo la kuwatafuta wahusika wa ubadhilifu huo ambao wamekuwa wakidumaza maendeleo ya watu wa jamii ya kifugaji.
Afisa mtendaji wa kata ya Ngoile Mereji Olepikok amekiri kupotea kwa fedha hizo na kwamba ameshafikisha taarifa hiyo kwenye vyombo vya sheria ili uchunguzi uweze kufanyika na kugundua waliohusika na ubadhirifu huo na hatua za kisheria ziweze kufuata mkondo wake.
No comments:
Post a Comment