Sunday, July 9, 2017

RAS Tabora apiga marufuku usafirishaji holelea wa mkaa



ewKatibu Tawala wa mkoa wa Tabora Dr THEA NTARA ameziagiza halmashauri za mji na wilaya katika mkoa wa Tabora kuhakikisha zinalinda rasilimali zilizopo ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji holela wa mkaa katika nje ya mkoa wa Tabora.
Akizungumza na wakuu wa Idara pamoja na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Katika kikao maalumu cha tathimini ya utendaji kazi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Dr THEA amewataka kusimama katika nafasi zao katika kuhakikisha wanalinda rasilimali zilizopo na kuhifadhi mazingira ambayo yanaonekana kuharibiwa kutokana na ukataji miti hovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa.
JACKOBO MTALITINYA ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega anaahidi kutekeleza maagizo hayo na kuhakikisha halmashauri hiyo inaendelea kuongeza mapato.
Uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti umekuwa madhara makubwa katika mkoa wa Tabora ambapo pamoja na mambo mengine umesababisha unyeshaji wa mvua kupungua kutoka millita 180 hadi kufikia millita 650.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...