Saturday, July 8, 2017

Mamba Mto Ruvuma tishio Mtwara, Waua watu 19 na kujeruhi 15 tangu mwaka 2010

chine-crocodileKwa takwimu zilizopo za kuanzia mwaka 2010 hadi sasa,mamba hao wameua watu kumi na tisa na kujeruhi kumi na tano.
Hakuna namna yoyote ya kuacha kufika katika mto Ruvuma ambao una mamba wanaokamata watu,kukosekana kwa maji ya bomba vijijini mwao vinawafanya wakazi wa vijiji jirani kutumia maji ya mto huo kwa matumizi yote ya binadamu. Tayari watu kumi na tisa wameripotiwa kuuawa na mbamba katika mto huo huku wengine wakipata majeraha na ulemavu wa kudumu.
Hamisi Mpunga ni mtoto na mkazi wa kijiji cha Sindano aliyejeruhiwa na mamba kwenye mkono wake wa kuume tangu mwaka 2013 akiwa anavua samaki anaugulia maumivu hadi sasa,huku wazazi wake wakikosa uwezo wa kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.
Serikali inaombwa kuwasaidia wakazi hao ili wasiendelee kuzulika na mamba katika mto wanaoutegemea kwa maji ya kunywa na shughuli za kilimo.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...