Friday, July 7, 2017

Muungano wa Saudia: Qatar ni tishio la usalama

Mataifa manne ya kiarabu, yanayoongoza masharti makali dhidi ya Qatar, yanasema kuwa, hatua ya Doha ni tishio la usalama
Mataifa manne ya kiarabu, yanayoongoza masharti makali dhidi ya Qatar, yanasema kuwa, hatua ya Doha ni tishio la usalama
Mataifa manne ya kiarabu, yanayoongoza masharti makali dhidi ya Qatar, yanasema kuwa, hatua ya Doha kukatalia mbali masharti hayo magumu dhidi yake, inaashiria nia yake ya kuendeleza sera ya kuhujumu usalama, katika eneo la mataifa ya Ghuba.
Kupitia taarifa ya pamoja, Saudia , Milki za kiarabu Misri na Bahrain, zimeonya kuwa, zitatoa hatua nyingine mpya na ngumu zaidi dhidi ya Qatar.
Mataifa hayo manne yalikatisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar mwezi uliopita, yakidai kuwa, taifa hilo linafadhili makundi ya kigaidi duniani, kama vile kundi la Muslim Brotherhood nchini Misri, na linashirikiana na hasimu mkuu wa Saudi- Iran.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, anasafiri hadi Kuwait kujadili namna ya kutanzua mtafaruku huo.
Qatar imerudia mara kadhaa kuwa, orodha ya masharti hayo, hayana maana kabisa, mojawepo ikiwa kufunga shirika lake la habari la Al Jazeera.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...