Friday, July 7, 2017

Mataifa sita ya Kiarabu yavunja uhusiano wao na Qatar

Mji mkuu wa Qatar, Doha
Mji mkuu wa Qatar, Doha
Mataifa sita ya Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Umoja wa Milki za Kiarabu na Yemen, yamekata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar yakiilaumu kwa kuvuruga uthabiti katika eneo hilo.
Nchi hizo zimeilaumu Qatar kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi, likiwemo kundi la Islamic State (IS).
Shirika moja nchini Saudi Arabia linasema kuwa taifa hilo limefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini, baharini na angani.
Lilinukuu maafisa wa Saudia wakisema kuwa hatua hiyo ni ya kulinda usalama wa nchi kutokana na hatari za ugaidi na itikadi kali.
Kile ambacho kwa wiki kadhaa kimekuwa kikichochea mzozo baina ya mataifa ya Ghuba sasa kimelipuka kuwa mzozo kamili wa kidiplomasia.
Katika tangazo la pamoja, Saudi Arabia ilikuwa ya kwanza kusema kuwa inavunja mahusiano yake ya Qatar mapema Jumatatu , mara moja ikafuatiwa na Bahrain, Muungano wa Milki za kiarabu Misri na Yemen.
Hatua za kwanza za mzozo huu zilionekana kujitokeza mwezi Mei wakati Qatar iliposema shirika lake rasmi la habari lilidukuliwa pamoja na kauli ambayo haikuwa sahihi iliyosemekana kutolewa na mtawala wake, iliyoonekana kwenye mtandao ikisifu kundi la wanawamgambo wa Iran na Lebanon la Hezbollah.

Taifa la Qatar

Mji Mkuu: Doha

  • 2.7 milioni Idadi ya watu
  • 11,437 sq km Ukubwa wa eneo
  • Kiarabu Lugha
  • Kiislamu Dini
  • 78.5 Umri wa watu kuishi
  • Riyal Sarafu

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...