Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba baada ya TCRA kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wa mawasiliano wakionesha hisia zao kwa kukerwa na matangazo yanayotokea wakati wa miito ya simu kabla ya kuunganishwa mpigaji na mpokeaji, ama wakati mpokeaji anapoongea na simu nyingine au mpokeaji akiwa hapatikani kwa wakati huo, kitendo ambacho ni cha kupoteza muda lakini pia kumpa mtumiaji wa simu matangazo hayo bila idhini yake.
Sambamba na agizo hilo, watoa huduma pia wameonywwa kwa kutoa matangazo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno bila ya ridhaa ya wateja wao kitendo ambacho ni kinyume cha matakwa ya kanuni za huduma za ziada mwaka 2015 na kanuni za kumlinda mtumiaji za mwaka 2011.
Aidha Mhandisi Kilaba amefafanua jinsi ambavyo kanuni za huduma za ziada zinawataka watoa huduma wazingatie.
No comments:
Post a Comment