Monday, July 10, 2017

Mh.Halima Mdee Apewa Dhamana

Halima

Mbunge wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Aliachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni kumi za Tanzania na kesi dhidi ya yake ikaahirishwa hadi Agosti 7, 2017.
Awali mbunge huyo wa Kawe alisomewa shitaka la kutimia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli
Mbunge huyo wa upinzani alikamatwa na kushikiliwa wiki iliyopita kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Ally Hapi ambaye alimshutumu Mdee kwa kumtolea lugha ya matusi Rais Magufuli.
Bi Mdee anadaiwa kutoa kauli za uchochezi alipokuwa akiongoza kikao cha Baraza la Wanawake Chadema jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...