Wednesday, July 12, 2017

Marekani na Qatar waafikiana kuukabili ugaidi duniani

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson (kushoto) akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani mjini Doha
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson (kushoto) akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani mjini Doha
Marekani na Qatar wamefikia makubaliano ya jitihada za kukabiliana na kudhamini ugaidi.
Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Doha na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ambaye yuko ziarani nchini humo.
Makubaliano hayo yanafanyika wakati ambapo Qatar ipo katika mgogoro mkali na majirani zake, ikiwemo Saudi Arabia.
Wote wamekata uhusiano na Qatar baada ya kuituhumu kuunga mkono makundi ya wapiganaji wa kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati.



Tillerson ameisifu Qatar kuwa ni nchi inayoupinga ugaidi
Tillerson ameisifu Qatar kuwa ni nchi inayoupinga ugaidi
Qatar imekana tuhuma hizo.
 Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, makubaliano hayo na Marekani, ambayo inasaidia kusuluhisha mgogoro huo, imeashiria kwamba inaiona Qatar kama mshirika mwaminifu katika mapambano dhidi ya ugaidi.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...