Saturday, July 8, 2017

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Vijiji 47 vyaelimishwa kutunza mazingira

571492875_orig
Tatizo la uharibifu wa mazingira ndani ya msitu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro Kinapa limepata ufumbu zi baada ya uongozi wa hifadhi kutoa elimu na hamasa kwa wananchi wa vijiji 47 vinavyozunguka hifadhi ya mlima huo juu umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira kwenye maeneo yao pamoja na msitu wa hifadhi hiyo.
Mhifadhi mkuu wa Kinapa Betrita Loibooki amebainisha hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku ta tu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika mjini Moshi, kwalengo la kuwaelimis a wajuwe kwa kina shughuli zinazofanywa na hifadhi ya taifa ,ili wakaelimishe jamii ,umuhimu wa kuyatunza mazingira.
Amesema mafanikio hayo ni baada ya na kumalizika kwa mgogoro wa mipaka kati hifadhi na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo, kutokana na alama za mipa ka zilizikuwepo awali kutoonekana vyema nakuilazi mu hifadhi kuweka alama nyi ingine kubwa ,pamoja na kuwapatia wanachi elimu ya uhifadhi wa mazingra pam oja na ujasiriamali.
Akifungua semina ya hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa hifadhi ya taifa TANAPA mkurugenzi wa uh ifadhi Mtango Mtahilo ameitaka jamii kushirikiana katika kuwafichuwa wanajihusisha na uharibibu wa mazingira, hali ambayo itakayosaidia kukomesha uharibifu huo ,nasiyo kiachia hifadhi ama serikali peke yake.

No comments:

Post a Comment

most viwed news

Uhuru na Lowassa waomba Wakenya kuvumiliana

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mgombea wa urais katika chama cha upinzani Chadema katika uchaguzi uliopita Edward Lowassa amewata...